Posts

Showing posts from August, 2017

mtandaoni shairi

Image
 Na Bin Zongo karibu mtandaoni uyaone ya duniani karibu keti makini ujue nani ana nini bando la uhakika bando halina shaka insta kunafikika twitter nakadhalika simu yangu smart tabu tabu sipati maridadi internet karibuni tuchart naanza nae Kimambi Mage haeshi vitimbi leo kapost mengi post zake hupingi alaani serikali ina nyingi dosari viongozi dhoflehali insta kote zohari mateja wazodolewa polisi wanatakiwa mkuu kashaamua mkoa kusimamia apost vita vyaanza biashara tokomeza harakati ndo imeanza madawa kuyamaliza wengine niwapinzani wameanzisha tafrani eti mkuu hajulikani amesoma shule gani mengi ya mtandaoni hufurahisha moyoni eti mchungaji gani amezaa kwa kuzini yule na wimbo mpya huyu na demu mpya mondi kaibua jipya bifu limeanza upya

PANDE MBILI ZAZOZANA

Image
Pande moja imevaa gauni ishara ya mwanamke nyengine imetinga kanzu ishara ya mwanaume! moja ya kanzu yasema wake waharibifu uaminifu hawana wamejawa mapungufu. gauni lataharuki almanusura livuke lasema hayasadiki waume wanachosema wao ndio mamruki uaminifu hawana. kanzu yatetemeka mate kinywani yatoka maneno yaropoka waume wametukuka, wanawake kwa vibweka duniani wasifika. Gauni latabasamu kwa dharau na kiburi lasema huna nidhamu mwanaume baradhuli ukishaishiwa hamu mwanamke humjali hauna ubinadamu wanaume ni zohari. Kanzu yakunja ndita mijicho yachomoka, kukupiga sitosita hivi ndivyo yaropoka sema nami kwa nukta dharau sitazitaka. Mwanamke gauni asema sikuogopi sitoshuka chini maneno yangu silipi tena yana thamani wanaume ni makapi. kanzu yagadhibika busara yamtoka matusi aropoka gauni lamcheka. Bi Gauni : tukana utukanavyo ila habari unayo, hivyo ndvyo mlivyo waume mapoyoyo, hasira zenye ujazo ni mapungufu hayo. Bwana Kanzu : wanitafutia kesi mwanamke hayawani ...