USISAHAU CHANGAMOTO @UjanaMajiYamoto

Na. Omar Zongo Ishi nami kwa furaha ila tambua siku moja kuna karaha hivyo usisahau kujiandaa! Usisahau changamoto ambazo kwa jicho langu naziona zimejaa pomoni! kupendana angali vijana ni suala lamaana lina taadhima na kubwa heshima! lakini usisahau kuwa ujana ni laana, jumba la usahaulifu na upotofu na kwa taarifa yako wengi waliouvamia sasa hivi ni wafu! walio hai wanasubiri andiko litimie!, afya zao dhalili, wakenda kama walevi, wamedhoofu mwili, nguvu zao kumbukizi, kwao naona dalili ya kupoteza nguvu kazi, ni baya suala hii UJANA kweli maradhi. Usisahau changamoto ya kwanza kwetu Ni Ujana! tena hii ni ya Moto yapasa kuomba sana. tuvuke mito, vijito tukeshe kuombeana! kwenye baridi na joto tubaki tumeshikana. Tena tuache utoto laa sivyo tutaachana. Ujana ni changamoto naomba kumbuka sana! wengi eti tulizo wanasema lipo kwa wazee! eti "vijana mzozo bora tuwapotezee" mapenzi sio mchezo yanaumiza aisee! singeni khabari hizo mchumba uzireje...