JUNIOR

"Sikuwahi kusimulia kisa cha kweli nikakiruhusu kusomwa na watu pengine hii inaweza kuwa simulizi yangu ya kwanza yenye ukweli ndani yake, ni zawadi kwa ndugu yangu Ramadhan Madebe ambaye kwa asilimia kubwa amechangia ukamilifu wa simulizi hii....ni sehemu ndogo pekee ndio yakubuni lakini mengi yana ukweli....." JUNIOR SEHEMU YA KWANZA Niliona wivu sana baada ya rafiki yangu kupewa jina na dada yako, yeye aliitwa mwinjuma lakini alimbeza jina lake hilo na akasema kuwa anapendeza zaidi akiitwa Geminus! Leo ndio nagundua kuwa aina ya familia bora kama ilivyo ya kwenu ndiyo huwaaribu watoto nakuwafanya wayachukie majina ya Kiswahili kutokana na wao kukesha wakitazama filamu za kizungu na kihispania. Hata kama muhusika mkuu katika filamu ya kizungu akitokea anaitwa Zongo, mradi ni mzungu na anacheza vizuri kwenye nafasi yake basi jina hilo linaweza kuwa ni jina zuri kuliko yote duniani. Kiukweli licha ya kuwa akili yangu ndogo lakini imebaini kuwa hili ...