CHUMBA HIKI USIFUNGUWE

Karibu mgeni wangu mwenye taadhima na heshima ilotukuka, Taarifa za ujio wako zilinifanya nikajiandaa vema kwa mapokezi. hakika nilisafisha nafsi, roho na mwili, niliyaonya matendo yangu dhalimu nikayakemea yasijitokeze kamwe nikiwa nawe. nilipojua waja niliandika waraka mreefu wa maneno ya vitisho kuziogopesha hisia mbaya zinitumazo kwenye zinaa nikaziambia habii!! zikae mbali nami kamwe zisinisogelee maana ni wewe ndio hupendi machafu yakaribie himaya yako. niliuonya ulimi uache kuropoka shombo, akili nikaihusia itulie katika kufikiri mema, tumbo nikaliambia liache kudai chakula mchana, ibada nikaziomba zije kuambatana nami ili kukukirimu. zile spika zangu chumbani zilizozoea kupiga kelele za muziki wa BONGO FLEVA sasa nikazifahamisha kuwa kuna KASWIDA nzuri za kina maherzain. Kitabu chenye maneno yaloshushwa ndani yako nikakiweka juu mezani, wallah tena naapa ukifika kwangu utakikuta juu tu kinakukaribisha. Sibishani kwa kupayuka tena. mara zote jirani ...