NAKUSHIKA SIKIO

Aliposikia hatua za mtu akaongeza umakini nakusogea karibu, ghafla akashtuka paji la uso wake likitobolewa na vyuma vya moto, alikuja kugundua baadae kuwa ni risasi ndio zilipenya kichwani mwake, mwili wake ulianguka chini mithili ya mzigo... ni hapa ndipo alipongundua SIKIO LAKE LIMEMPONZA kusikiliza hatua za watu hatari na wakatili kiasi kile....alijilaumu kwanini asingepuuza kusikia hatua zile lakini majuto yake hayakuweza kusaidia roho yake isitoke...sasa alikuwa chini akipigania roho yake ambapo dalili zote za kifo tayari aliziona... SIKIO LILIPONZA ROHO YAKE! nina kila sababu ya kuzungumza na SIKIO LANGU!. Nakushika sikio! Na Omar Zongo Sikio langu ni dira nzuri ya kuupima muelekeo wa ngurumo za sauti zitokazo pande zote za dunia hii. leo nasema nawe sikio maana namini wewe ndio kiungo pekee ambacho utanifanya ule umimi niliozaliwa nao, nisiupe nafasi kuwa kero kwa wengine. usikasirishwe na mabezo ya watani wangu wanaodai nina sikio kubwa ka' upawa wa uji,...