Posts

Showing posts from March, 2017

UJUMBE KWA WAKWE ZANGU

Image
 ''Katika dunia yetu ya leo malezi ni suala ambalo halipatilizwi sana, wazazi wamekuwa wapuuzaji hivyo kufanya vijana wa kiume kutotambua maana ya uanaume wao na vijana wa kike   kutoiona thamani yao, kama muandishi nimeona haja yakukumbushia suala la malezi kwa mtindo huu...ifuatayo ni barua kwa wakwe zangu'' Na BIN ZONGO Bado sijaoa lakini naamini ipo kaya moja duniani hapa anaishi mwanamke nitakayemuoa na pengine analelewa na wazazi wake Ujumbe huu nataka ufike kwao... Ujumbe huu uwafikie wakwe zangu na najua mtastaajabu sababu bado binti yenu hamjamuozoesha wala pia barua ya posa hamjapokea. me naamini ninyi ni wakwe zangu na sitasita kuwaita hivi sababu wahenga walisema NDOA HUFUNGWA MBINGUNI. mimi na binti yenu tayari tumeshafunga ndoa mbinguni hata kabla nafsi zetu hazijaletwa hapa duniani. nimewahi kuwaletea waraka huu wa barua ili kuwajulisha mengi ninayoyataka muyafanye kabla sijakutana na binti yenu. naandika ujumbe huu nikiwa sina hata...

MFALME WA THAMBO

Image
''Imepitia mengi kabla yakuwa nchi yenye kuheshimika duniani, busara zilitumika na hatadamu za watu wengi waasisi wa taifa hilo zilimwagika, historia inaonesha ni miongoni mwa mataifa ambayo yamepiia changamoto nyingi sana na mfalme wa sasa anatimiza idadi ya wafalme 19 waliowahi kuitawala nchi hiyo iitwayo THAMBO' ' Na Bin Zongo "Mwanangu huyu ni mpendwa nampenda toka moyoni, nashangaa mnavyomponda hata haya hamuoni, acheni mambo ya kijinga hapa kazi hebu fanyeni siendeshwi na propaganda mie ni baba najiamini..." Hayo ni maneno ambayo aliyatoa mfalme kwa mwanae wa mwisho ambaye alimpa ucrown prince bila kujali kuna mtoto wa kwanza ambaye kisheria alistahili yeye ndiye awe crownPrince(mrithi wa mfalme). kwa sababu ambazo mfalme mwenyewe hakuziweka wazi alikuwa akimkingia kifua sana mwanae huyo wa mwisho. majigambo na mavuno vikamtawala, kiburi kikamgumbika hakujali tena kujenga uhasama na watu mbalimbali tena wazito katika utawala wa baba yake....

AUDIO YA SIMULIZI JICHO VUMILIA

Image
Hii ni moja ya simulizi yangu BORA niliyoiteua kwa mwaka uliopitwa inaitwa JICHO VUMILIA, isikilize kwa sauti nikikusimulia kwa Utashi na weledi wa hali ya juu..

UTENZI WA MAHABA

Image
''Zawadi ni chachu ya mahusiano ya aina yoyote ile, mzawadie ulicho nacho yule ambaye unahisi ni sahihi kuzawadiwa nae, naamini tabasamu lake usoni ni ishara tosha yakufarijiwa na zawadi uliyompa, kuna aina nyingi za zawadi, lakini katika mapenzi Maneno matamu ni zaidi ya zawadi zote unazozijua wewe, waswahili huamini NENO HUUMBA......'' UTENZI WA MAHABA Na Bin Zongo leo nachana kifua nautoa moyo nje nataka kuyaachia yalo ndani uyaone si joto wala baridi ni wastani kipupwe leo nataka kuahidi ukweli wangu nikupe kupenda kama umbea masuto nastahili naapa sitokimbia majivu ntayakubali laa kupenda ni homa matibabu weka mbali nataka kuumwa homa joto mwili liwe kali mapenzi kama ugali mpunga mie wanini sitaitaka zohari mahindi weka chumbani kupenda jambo geni sijawahi kabla yako naapa kwa rahmani nafsi yangu mali yako mwenzako kwetu pwani kudekeza nimefunzwa kuoga nawe bafuni Tanga nimesisitizwa kupiga ni ukatili u...

MAJIBU YA BARUA YAKO MAKAYULA

Image
''Nimeipata nafasi yakujibu salamu zako ulizoniandikia Makayula. sina shaka utaniambia mbeya wangu ninani" Na Bin Zongo Mpaka kuandika waraka, najua umesalimika Afya yako sina shaka, nilipo nina uhakika. taharuki imenifika ,yanigubika mashaka. ninani mbeya wangu, Makayula nieleze. Urafiki nishakataa, wanafiki waja waleo Mabingwa wakuhadaa, sikitaki icho cheo Waraka nimeshangaa, usemayo yote siyo ninani mbeya wangu, Makayula nieleze. Nyumba yangu ipo sawa, amani iko pomoni Fikira hasi ondowa, zibakishe tu moyoni Sisikie yakuambiwa, mengine ni ya kubuni Ninani mbeya wangu, makayula nieleze. Mie ni yuleyule, watangu tungali shule Haiba yangu upole, sijayaiga ya wale Ndoto zangu zilezile, kesho nifikie kule, Ninani mbeya wangu, Makayula nieleze. Umechotwa na mtego,umevalishwa hasara Wamekugeuza zigo, kukupa habari uchwara Hebu liambae pigo, kwa kusimama imara Ninani mbeya wangu, Makayula nieleze. Shemejio ana raha, mie tunda la peponi Kwake hakun...

SALAAM BIN ZONGO

Image
''Katika kuenzi tenzi na ushairi, moja ya vijana wa leo ambao nawaheshimu sana katika utenzi ndugu yangu Fulgency Makayula, ameamua kuogelea katika bahari ya ushairi kwa kuonesha uwezo wake wa tenzi kwa kuandika ushairi huu ndani yake wenye dhima ya barua inifike....sina shaka haina uhalisia wowote na kweli bali ni katika kuonesha ushababi wake katika tenzi....HAKIKA NAKIRI AMENIPA CHANGAMOTO KATIKA KUJIBU UTENZI HUU'' Kwa kheri zake karima, natumai u buheri Na mimi wa afya njema, tena nina mpya ari Nimesharudi salama, kwa ile ndefu safari Salaamu bin Zongo, nisalimie Handeni Ni miaka mingi sasa, na sikukuandikia Kama vile tuna visa, kumbe tu kufikiria Urafiki namba tasa, mimi nawe hesabia Salaamu bin Zongo, nisalimie Handeni Isome barua hii, bin zongo usipuuze Nitapata kufurahi, akisoma na Rupaze Nitakuja nikiwahi, nikuletee na zeze Salaamu bin Zongo, nisalimie Handeni Rafiki yangu wa damu, umeponzeka na nini Nimeyasikia magumu,yanipa upunguwan...

DUBWASHA

Image
Na. Bin Zongo atokapo ni gizani meusi mavazi yake usoni haonekani kuua ndo kazi yake ameagizwa na nani siri kubwa jibu lake wamfatao hatiani mateso ndio hila yake wengi sasa kitanzini wachini hata wajuu wengine wa kaburini kwakuyataka makuu hali tete duniani roho zote juu juu mwenyeji wake ni nani hiyo ndio siri kuu awahadaa vijana nguvu kazi ya taifa nusura yake hakuna watu wengi washakufa wazee pia vijana kawamaliza kwa sifa yaleo sio ya jana hali sasa inatisha sumu yake ladha tamu ukiionja wanogewa inachanganyika damu hutaacha kurudia kila mara una hamu kuipata na kubwia mgeni mwanaharamu vijana wateketea sababu zao dhaifu eti hali ngumu chanzo afya zao kama gofu hawalioni tatizo wanakaribia ufu lakini sio kikwazo matumizi maradufu kuyaondoa mawazo dubwasha jingi la hila lateketeza kizazi ukithubutu kulila kuliacha tena huwezi lina nyingi sana hila vazi lake ubazazi maombi kwako mola muondoshe mpuuzi afrika mpaka ulaya kape...

Twasubiri BIN ZONGO

Image
Lile eneo la Dhania, eneo la kufikirika, eneo tata lenye mashaka na nyingi Hadithi, eneo lakusadikika ndilo nalizungumzia hapa. Eneo ambalo mababu na watu wote wakale mpaka wa leo wanalitambua kwa jina moja tu 'MBINGUNI' eneo hili ndilo limesheheni katika simulizi hii muktasi yenye kusisimua na kukujulisha thamani ya simulizi zangu adhimu ambazo daima dumu ZINAISHI na nafarijika kila uchwao lugha adhimu yakiswahili ikiendelea kunithibitishia uhai wa MILELE WA SIMULIZI HIZI hakika naamini uhai wa simulizi hizi ni DAWAMU hazitakufa abadani. Na. Omar Zongo katika anga la mbingu lenye mapambo ya rangi nzuuri yenye kuvutia inayotambulika kama buluu kulionekana vivuli vya mawingu meupe yasiyo na umbile maalumu! mawingu yale yalivinjari kwa mbwembwe yakionekaba kujongea kutoka sehemu moja kwenda nyengine. Binaadamu yeyote makini ambaye ameruhusu macho yake yakatuwama angani kwa muda huu sina shaka ataona purukushani za mawingu kujongea kwa maringo, sina uhakika kama kinachoo...