JIKANE SASA

''jikane kwa pigania maneno kama vile anaringa, ana roho mbaya maana maneno hayo tafsiri yake ni nzuri kwa nafsi yako yaani nikwamba unajiamini na njia zako na unapambana kwa mafanikio yako kwa kushirikiana na wachache ambao utaamini wao wanakustahili, unaendana nao na wana msaada mkubwa wakukufikisha unapoota kufika'' Na. Omar A. Zongo Waheshimiwa wahenga walisema kuwa utendapo wema, nenda zako kamwe usingoje shukurani. wakaibuka wengine wakatanabaisha ni busara mkono wakulia ukitoa wakushoto usibaini. wakaja wengine wakaunga mkono kwa kusema wema wa aina yoyote hauozi. ahsante waheshimiwa wahenga, nasadiki lakini zaidi naheshimu mawazo yenu yalo busara pomoni. kilembwe wenu leo naibua hoja ikiwa ni namna nzuri yakuheshimu fikra zangu nakuzithamini maana nimejaribu kuangaza dunia yote hii sikuona wakuweza kuthamini mawazo ya wengine maana ni watu wa dunia hii ndio walio jaaliwa dharau nakujiona wao na watu wao wanaowahusu ndio bora kimawazo. sijawah...