Posts

Showing posts from January, 2017

SHEMEJI WA.COM

Image
'Shairi lifuatalo ni utenzi wakubuni haujaakisi tukio wala kisa chakweli kutoka kwenye jamii, utenzi huu unaakisi hali ya maisha yalivyo kwa sasa na undugu usivyo na thamani katika mapenzi' Na. BIN ZONGO alinifata chumbani muda natoka kuoga akanivaa mauongoni ukanitawala woga nguo kazitupa chini shemeji wa dot.com kaka yako hayupo kasafiri kitambo shemeji jilie vyako usizilete Tambo nina haja mwenzako shemeji wa dot.com ndani mimi nawewe wengine hawatajua shemeji haki nipewe nateseka wajua nataka nishughulikiwe shemeji wa dot.com butwaa lanipumbaza naota ama nikweli kichwani najiumiza niache au nikubali shetani kampumbaza shemeji wa dot.com umbo lake namba mtupu maungo yake kaidondosha khanga aibana sauti yake dhamira kaipanga shemeji wa dot.com hatunazo tena nguo nikama tumezaliwa ni lipi langu chaguo shemeji asisitizia nasita kusema sio shetani kasimamia shemeji wa dot.com anivuta kitandani naanza kujilaumu kuna mtu mlangoni...

JANA NILIKUOMBEA

Image
'Yafutayo ni maneno yakubuni hayana uhalisia wa kweli, ni maneno kuhusu mapenzi na usaliti uliosheheni katika mahusiano ya kileo' Na. Omar Zongo Nimestaajabu sana kushtuka usiku saa tisa bila sababu ya mana eti mapenzi ndio kisa. Hofu sauti za usiku na ndege wa ajabu ajabu, kelele za vyura na bundi zilishindana, kiza ndani ya chumba ilikuwa balaa sana. isingekuwa kuniacha ungekuwa pembeni yangu nina uhakika ujasiri wa kiume ungeongezeka maradufu nisingeonesha kuogopa ningejikaza. ningeigiza kukulinda nisingehitaji unidharau ningekuondoa woga ili unipandishe dau. ni ule mgogoro wetu ndio umefanya niwe mpweke, niukumbatie mto wangu na huu ubaridi unipige. sijui ni upendo wangu ndio ulifanya uniadhibu au ni ule upole wangu bado sijapata jibu. mbona nilikupenda sana na heshima lukuki sikutaka uwe mpenzi bali mchumba wa heshima. au ni ule upofu wangu ndio ulinifanya nisione, upofu wa mapenzi yangu ndio ukageuka pakashume, ukaugueza utu wangu kuwa kituko mbele za wa...

TATIZO NAKAZA SANA

Image
"Zongo nakubali sana uandishi wako ila tatizo unakaza sana" jamaa flani ananitext kwa inbox, naisoma text yake naitafakari najikuta nacheka mwenyewe sababu kutafakari kwangu kwenyewe nilikuwa nakaza sana kama vile nafikiria issue nguuumu! najikuta kicheko chakujicheka mwenyewe kinanikamata mwisho naishia kutabasamu badala yakucheka kabisa, najicheka huku najipiga kibao kidogo cha utani huku nikijiambia "zongo unakaza sana" kama mbabu wa miaka mingi hahaa! poah leo sikazi wala sitaki kabisa masuala ya kukaza mana hali yenyewe ya maisha kwa sasa imekaza automatically so namimi nikijifanya naandika kimkazo nitazidi kufanya mambo yawe magumu! Nimesema leo sikazi naongea lugha yetu tunayoelewana vijana mtaani! story yangu yaleo iko hivi, jamaa angu, damu yangu, chafu yangu yani mwanangu kinomanoma zaidi nikisema jembe langu ndio utanielewa, jina sio lazima sana ila kitu cha msingi ni kajisehemu kadogo sana ka tabia yake ambako kanamfaya baadhi ya i...

SHAIRI: SIKU ITAISHA

Image
'Shairi lifuatalo linalenga kutoa faraja kwa masikini anayeendea kukata tamaa ya maisha mwenye kudhani kuwa hakuna namna ya yeye kushinda vikwazo vya maisha magumu ya kila siku, MUNGU YU PAMOJA KATIKA HARAKATI ZETU ZA SIKU ZOTE' Na.  Bin Zongo 1: moja ndio saa dakika kadhaa naamka nakaa tumboni nnanjaa hii siku itaisha 2: mawazo yajaa kichwani balaa dunia hadaa nna dhiki na njaa hii siku itaisha 3: miale yaangaza siku mpya yaanza ntaishije nawaza dhiki zanimaliza hii siku itaisha 4: nakiacha kitanda sinapo pakwenda naanza kupanga vipi ntashinda hii siku itaisha 5: mtaani nadaiwa luku ni zamu yangu kooni nimekaliwa yaniponza hali yangu hii siku itaisha 6: kuoga bila sabuni sijui naoga nini mikosi mwilini sinayo amani hii siku itaisha 7: chumba cha uani karibu na chooni asubuhi foleni kumejaa pomoni hii siku itaisha 8: toka basi uani asemavyo jirani mekawia chooni usoni nina soni Hii siku itaisha 9: narejea chumbani...

SURAYE NAIKUMBUKA : SHAIRI

Image
'Utenzi ufuatao ni moja ya ishara yakukumbusha watu kuthamini kila mtu maana wahenaga hawakukosea waliposema SICHAGUI SIBAGU ATAKAYENIZIKA SIMJUI, aidha pia somo la kutomdhania mtu mabaya linagusiwa katika utenzi huu Adhimu' Na, Bin Zongo ndani ya daladala kanilipia nauli kauepusha msala konda ni baradhuli suraye naikumbuka ila jina simjui ilikuwa ni patashika ingekuwaje sijui sikuwa nakupashika abiria siwajui suraye naikumbuka ila jina simjui alikaa pembeni yangu hata sikumsalimia nilijua mambo yangu wala sikumzingatia suraye naikumbuka ila jina simjui konda adai chake nauli azikusanya natazama ili nimpe hapo naanza kuhanya suraye naikumbuka ila jina simjui natazama mfukoni nauli yangu siioni aibu aibu gani nauongeza umakini suraye naikumbuka lakini jina simjui damu yangu nakonda zilishakataana tangu naanza kupanda tulikuwa twarumbana naanzaje kumpanga yakwamba nauli sina suraye naikumbuka ila jina simjui oyah nipe nauli konda ...

CHANDA CHA PETE

Image
Nina jivika upofu, kwa navyo shindwa tazama Kwa mawazo yangu nyofu, fikara sizo chutama Hakuna cha upotofu,   jicho pevu kutazama Azima ya moyo wangu, chanda cha pete fikiri Chanda nilikuchagua, moyo wangu kutiisha Tena nilikubagua, kwa misingi ya maisha Kama jua limetua, joto umelikatisha Azima ya moyo wangu, chanda cha pete fikiri Wewe ndiye   wapekee, kwa ndugu zako watano Ukipenda nikemee, ntajifunza kwa mifano Sikupenda ulegee, tena niliuma meno Azima ya moyo wangu, chanda cha pete fikiri Chanda changu kitulivu, usie penda mapuro Najua u msikivu, na usiyetaka kero Yakatae machakavu, yamenipaka uchuro Azima ya moyo wangu, chanda cha pete fikiri Ni wapi nilikosea, hata nashindwa kung’amua Kule niliko potea, ni vipi nitagundua Mbona nilikupepea, kwa huba njema za dua Azima ya moyo wangu, chanda cha pete fikiri Mimi nilifunga nia, kwa penzi loshikamana Nilifurahi kuingia, kwa pendo la kujichana Siri sikujifichia, nilikuwe...

MIMI NI BORA

Image
Mimi ni mimi, wewe ni wewe, mimi ni jasiri, mbunifu, mtulivu, nina akili nzuri, mkweli, naheshimika hakika MIMI NI BORA! Naishi maisha yangu, sina tatizo,nina furaha, najipenda, hakuna kama mimi, MIMI NI BORA ZAIDI. Napenda ninavyoishi, sina mawazo, nina furaha naweza kukupokea ukinihitaji nakukupuuza ukinitenga, yaani ilivyo ni kwamba wewe ni nafsi yako nami ni nafsi yangu, wewe hauna nafasi katika himaya ya amani na furaha ya MOYO WANGU! kama wewe una thamani hiyo ni ya kwako wewe na wanaoamini una thamani, mimi hainihusu!, naiona thamani yangu pekee, thamani yenye ubora usiolingana na yoyote. mimi nimebarikiwa, hakika mimi ndio mimi, kama mimi atoke wapi!? mimi sio masikini, umasikini haufanani na mimi, mimi ni mtu mzuri, uzuri wangu duniani mfanowe hakuna. mimi siijui shida maana shida hua naipuuza, naiweka kushoto natinga koti la ujasiri, napiga hatua za kujiamini naisogelea juisi ya bariidi iitwayo furaha nainywa kupoza koo langu. mimi sura yangu inapamb...

TUMAINI LIPO

Image
Kila siku mpya napata tumaini jipya hasa ninapouchunguza mwili wangu nakubaini hauna hitilafu yoyote ya maradhi, nashukuru nakuamka nikiwa na amani licha ya kwamba sina uhakika wakifungua kinywa, tumaini langu laniambia leo ndio siku ile ya mapinduzi ya maisha yangu. siku ya kugeuza mawazo kuwa vitendo, siku ya ahadi kutekelezeka, siku ya nuru mpya katika kiza cha ufukara na maisha ya bahati nasibu. naamka kwa miruzi, salamu zenye bashasha kwa majirani, utani wa hapa na pale pamoja na ucheshi unanifanya nionekane mwenye furaha nisiye na shida, mtu niliyeridhika na maisha, hakuna ajuae siri ya amani yangu!. natembea kwenda kwenye mitego yangu, njiani nakutana na wengi waliokunja sura zao kana kwamba hawakufurahia kuamka kwao. natamani kuwaambia watabasamu hata kidogo lakini nashindwa nabaki kuwatazama mimi kwa tabasamu huku nikiwasalimia kwa furaha. wananijibu kama mimi ndio chanzo cha matatizo yao lakini sijali, naendelea kutabasamu nikiamini kuwa ile ni siku mp...

IGIZAUKAMILIFU 2017

Image
kwanini uigize ukamilifu mwaka 2017? sababu ni hizi........ Na. Mr Experience Udhaifu wako ni moja ya sifa zinazo kutambulisha kuwa wewe ni binaadamu lakini haimaanishi kuwa ndio uutangulize mbele nakuwa muumini wa makosa. anza sasa kufikiri kuigiza ukamilifu katika kila jambo. pengine hali ni ngumu umezongwa na majukumu! kipato hakiridhishi na umeandamwa na kila dhiki duniani hapa, acha nikwambie kuwa udhaifu nikusononeka nakuacha mawazo yakutafune taratiibu ndani yako. unaonaje sasa ukianza maisha mapya kwa kuvaa vazi la ukamilifu, kujiveka tabasamu la kuridhika hata kama unateseka. lengo nikuficha wengine wasijue dhiki zako, wasiyajue maisha yako, wasione kuwa dhiki inakuchapa nawe unachapika. Igiza ukamilifu, weka tumaini mbele hakika nakuambia utakujia ukamilifu kwa kuuishi ndani yake. ndio fukara lakini unatabasamu, huchoki kutafuta, unaamini katika pumzi na uzima wako na unaishi maisha yanayompendeza yoyote kwa kumjali kwa hali maana mali huna, hakuna kitakacho...