KWAHERI 2016 ; SHAIRI

Ni mbali ulipotoka kamili umekamilika tamati imeshafika wajibu kukuimbia safari si lelemama mengi tumeyaona mengine yametuuma ni wewe umetuletea sifayo sasa ukongwe ujana hunao tena yakupasa tu uende andiko limetimia wapo wenye simanzi umewaachia jeraha uliwatoa machozi ishawekwa historia tamu yako na shubiri vyote tumeviona umekuwa mashuhuri jua kupatwa mchana tetemeko la kagera tanzia tanzania umetutia hasara uendapo salimia kifo kilifanya yake mwaka ni mrefu sana hivyo ni desturi yake sote twaelekea furushi lako la rushwa rudi nalo jeupe sasa utawala mpya hauitaji uzembe Tunza macho ya Side scopion alikupa hongera pia kwa ubabe kumuua rais wa Cuba Miili ile mtoni waijua siri yake na vipi kuhusu John Faru kufichwa kwake Afrika ya upinzani viongozi kushika dola Uchaguzi Marekani Trumpel Mr. Hongera. Mitandao imeonyesha walimu wagawa dozi wanafunzi Na shisha Hawaishi uchokozi maisha na mziki usukuni weka pembeni dereva...