Posts

Showing posts from October, 2016

NGUVU KUZIMU& UDHAIFU DUNIANI, IZRAEL NAOMBA TUYAJENGE!

Image
BY, Omar A. Zongo Izrael Mtoa roho nianze kwa kukupa pongezi, hakika Kazi yako umeifanya kwa ufasaha  kuzimu kwapendeza! nami niseme Ahsante kwa kunialika karamu hii ingawa umenisimamisha langoni lakini yumkini naona ndani sina kinyongo, nimeridhika na mwaliko wako! Izrael wewe ni jemedari bingwa wakuchagua vizuri maana hafla yaendelea ndani lakini navutiwa na jinsi kuzimu ilivyo pambwa naamini ni kazi ya akili yako kuwachukua wapambaji mahiri kutoka duniani! maandishi yamepambwa kwa umahiri kutambulisha kuwa hii ni NYERERE DAY! Sina shaka aliyeandika maneno haya kwautashi ulimnyakuwa toka duniania ingawa sijui ni ninani hasa! jukwaa la kuzimu limepambwa kwa mbadilishano wa sauti za wanamuziki wa kila aina TX MOSHI kwa mziki wa dance akiongoza wanamuziki wenzake wengi kutoka kongo namuona kwa mbaali PAPA WEMBA hakika izrael umeimaliza dunia kama ikitokea karamu kama hii duniani wakali hawa hawapo tena waliopo wanafanya kawaida sanaaaa. Nasikia kuzimu SIASA yake safi hai...

CHIZI MAFANIKIO SEHEMU YA 4

Image
ILIPOISHIA Bi getrude anasukumwa nakuanguka chini, huku mama yake salim akikimbilia ndani huku analia, tayari mawazo mabaya yalishamuingia kuhusu kifo cha mwanae_ SASA ENDELEA... Alijisikia vibaya sana kusukumwa namna ile, alijiokota taratibu nakukaa kitako kabla hajaamka nakuanza kumfuata nyuma mama yake Salim. tayari alishaona dalili mbaya ya chuki ambayo mara zote aliomba isijitokeze katikati yao hasa kuhusu kifo cha Salim. alijisikia vibaya sana Bi Getrude, aliona namna ambavyo dunia inamgeuka ghafla. hatua zake ziliishia kwenye mlango wa chumba alichoingia mama yake salim. ulikuwa umefungwa kwa ndani, alijaribu kugonga mlango nakumsihi afungue lakini maneno aliyojibiwa ndio yalimuumiza zaidi. na alisita hata kuendelea kugonga mlango ule. " Kamwambie mwanao aje animalize namimi, sioni thamani ya kuendelea kuishi kwakweli mwambie aje aniue kama alivyomuua Salim wangu, alikuwa na makosa gani masikini mwanangu" kutoka ndani yalisikika maneno haya, ilikuwa ...

NAISIKIA MILUZI

Image
Hekaheka zachachama,kelele huko nyikani Dawa ya chachu kutema, isibakie  kinywani Usibaki kutetema, ukavimbiwa tumboni Nyikani  kwa tanda giza, naisikia miluzi   Nyika iliyo salama, hii miluzi ya nini Kukiepuka kihama, hiyo miluzi acheni Mioyo yote ya nyama, kutishana kwa fatani Nyikani  kwa tanda giza, naisikia miluzi Ebu simameni hima, acheni usubihani Tulimuomba Karima, atupatie aghani Tukapewa ilo vema, naomba tuitunzeni Nyikani  kwa tanda giza, naisikia miluzi Ukivalia pajama, huku machozi usoni Utapata tu lawama, nyika ikiwa motoni Tuende tukichechema, tutunze mali nyikani Nyikani  kwa tanda giza, naisikia miluzi Miluzi isiyo mema, yatanda masikioni Hakuna hata la wema, upoto sio kifani Tumezaliwa kusema, ila busara pimeni Nyikani  kwa tanda giza, naisikia miluzi Mbele tusirudi nyuma, tukachekwa na wageni Tujengane tu  kwa wema, hekima za duniani Tukithubutu simama,tutaishia jangwani N...

KWENDRAAA

Image
Hii ndio nguvu yawaandishi, neno lolote huweza kuwa mada pana na ikajenga mvuto kwa yoyote.... leo ninalo neno hilo lakiburi na jeuri ambalo limeathiriwa kutoka kwenyeneno adhimu lakiswahili linalotamkwa kwenda. vijana wakileo wajuaji waso na mipaka wenyewe wanatamka kwa dharau na mashushu wakisema kwendraaa.... nifanye nini nami ni nafsi inayoishi leo, nafsi ambayo haiwezi kuepuka kutamka neno hilo kwendraaa... leo nalitumia nasema kwendraa, toka mbele yangu fisadi wa huba, usiyejua nini maana yamapenzi. nafsi ikusute suto kuu la kuzodoa matendo yako haramu uliyoyatenda kwangu licha ya upendo wangu imara niliyokukabidhi bure. nasema kwendraa sina haja nawe popo mtafutaji hata vilo katazwa na Mungu! natafakari siti ya daladala naona wafanana nayo maana niwewe ndiyo huruhusu kukaliwa na yoyote mradi tu awe na shilingi yakukulipa. kwendraa mwana kwenda hunifai kwa kulumangia wala kulia nakachumbari. iweje nguo yako ya ndani iwe busy kuvuka kama walipwa mshahara kwa zoez...

NAOGOPA

Image
S auti ya Bwana Said yajirudia kichwani mwangu yanisononesha mno, namsikia akisema "nilikuwa tayari kumuachia pesa na kila nilichokuwa nacho mradi aniache mzima lakini haikuwa hivyo, alinishambulia nakunitoa macho yangu kabla sjapoteza fahamu nakutoelewa kinachoendelea" sauti yake yakujuta kupita buguruni siku ile bado yanirudia kichwani mwangu dukuduku la uchungu lanikaba, huruma yanikumba lakini zaidi sura mbaya ya dunia naiona machoni mwangu nawaona walimwengu wenye roho mbaya, wakatili mikononi wameshika silaha za ajabu wakiwawinda binaadamu wenzao usiku na mchana. natazama pakukimbilia sipaoni nabaini kuwa duniani sio mahala salama tena pakuishi, hofu yanitawala huku nikijitajidi kupingana nayo ili niendelee kuwa jasiri lakini naona sura za wakatili zikizidi kuongezeka zote zikinitisha na matendo yao.  taratiibu naanza kubaini kuwa sina jinsi yanipasa tu niwe mpole nanikiri kuwa NAOGOPA. naogopa sana tena sana! maana hakuna pakukimbilia wala hakuna wakunitetea...