SITAKUSAMEHE

Leo nimekuomba uketi chini nikufunulie tena kwa mara nyengine jarada hili lenye kanuni zangu na muongozo muhimu kwa mchumba angu! jarada hili lina kanuni Hamsini jiandae kujua leo nasoma kanuni ya ngapi maana mara ya kwanza nilikusomea kanuni ya Sita niliyoipa jina la NITAKUOA LAKINI SITASAIDIA NDUGU ZAKO! hii leo nimepata mshawasha wakukusomea kanuni ya Kumi yenye kichwa cha habari chenye neno moja tu SITAKUSAMEHE. kubwa na muhimu tambua kuwa nitakuoa kamwe sitaruhusu maneno yangu haya yakumbwe na kimbunga kiitwacho AHADI HEWA. Nitahakikisha nakuoa na nasimamia furaha yako muda wote ndani ya ndoa yetu! ule ukatili wa mwanaume kumpiga mkewe mpaka kumpa chongo kamwe sitauruhusu univae nakunilaghai, ukinikera nitakutandika na maneno yakukuonya na ukiendelea nakucharaza na dua yenye maombi mazito kwa mola wangu nina imani kupitia yeye aibu yakuniudhi nakunikaraisha itakuvaa na utaona haya kunipa mateso mtoto wa mwanamke mwenzio. yote nitayafanya mchumba kuhakikisha unajivunia...