BURIANI BI SHAKILA

Hakika kila mmoja anaweza sema lake kuhusu ujumbe huu! ila mimi sitajibu hayo yote nitajibu kuhusu huyu atakayesema kwanini nimechelewa kuomboleza na hata kutia neno kuhusu kifo chako mpaka siku kadhaa sasa zimepita. Burian Bi Shakila na hakika wanazidi kuniliza hawa waja kwa swali hili na kabla sijaendelea kukuaga acha nisemezane nao hivi Ningewazaje kutia neno katika msiba mzito kama huu, msiba uliogonga moyo wangu nakunipa ganzi katika viungo vyote hasa ulimi unaomfanya mtu atamke. ni mikono hii ndiyo iliyoshindwa kabisa hata kunyanyuka nakuipungia mkono wa kwaheri nafsi ya Nguli huyu wa Muziki wa taarab iliyokuwa inapaa angani taratiibu huku ikisonona kuona Taarab asilia waasisi wake wanaisha katika ulimwengu huu. ni macho haya yakwangu Bin Zongo ambayo yalishindwa hata kudondosha chozi ilhali moyo ukiwa umetota kwa huzuni ya msiba ule, hakika yalikuwa maajabu mpk jicho kushindwa kulia kwa mshtuko wa habari hii yatanzia. kama viungo vyangu vilishtushwa na msiba ule nin...