Shaaban Robert Katabasamu
Siku kadhaa zimepita tangu niandike barua kwa marehemu nguli wa Kiswahili na mtunzi wa mashairi Sheikh Shaabani Robert, Usiku naweweseka nashtuka nakiona kivuli cha Shaaban Robet, kinanikabidhi Barua, kisha kinatoweka machoni mwangu , napigwa na butwaa, nakurupuka kana kwamba nimemwagiwa maji ya baridi naikimbilia taa naiwasha , mkononi mwangu nauona waraka ule wa barua niliyokabidhiwa, moyo unaenda mbio, macho yanakimbilia kusoma kilichoandikwa! Maneo ya juu kabisa yameandikwa. Shaaban Robert Katabasamu! Naongeza umakini kusoma zaidi…. iliandikwa hiviii. Asante sana, kilembwe changu, yumkini baadhi ya kizazi chenu chatambua niliwahi kuwapo duniani basi najifaghiri sana huku nilipo. Barua yako nimeipokea, ingawa hukuipa jina barua ile ila nikaona nisifanye kosa kama ulilofanya wewe yakwangu mie nimeipa jina hilo hapo juu, Shaaban Katabasamu. Kwa hakika umenifanya nitabasamuj kwa mara ya kwanza tangu kufariki kwangu, mwanzoni niliv...