Posts

Showing posts from 2016

KWAHERI 2016 ; SHAIRI

Image
Ni mbali ulipotoka kamili umekamilika tamati imeshafika wajibu kukuimbia safari si lelemama mengi tumeyaona mengine yametuuma ni wewe umetuletea sifayo sasa ukongwe ujana hunao tena yakupasa tu uende andiko limetimia wapo wenye simanzi umewaachia jeraha uliwatoa machozi ishawekwa historia tamu yako na shubiri vyote tumeviona umekuwa mashuhuri jua kupatwa mchana tetemeko la kagera tanzia tanzania umetutia hasara uendapo salimia kifo kilifanya yake mwaka ni mrefu sana hivyo ni desturi yake sote twaelekea furushi lako la rushwa rudi nalo jeupe sasa utawala mpya hauitaji uzembe Tunza macho ya Side scopion alikupa hongera pia kwa ubabe kumuua rais wa Cuba Miili ile mtoni waijua siri yake na vipi kuhusu John Faru kufichwa kwake Afrika ya upinzani viongozi kushika dola Uchaguzi Marekani Trumpel Mr. Hongera. Mitandao imeonyesha walimu wagawa dozi wanafunzi Na shisha Hawaishi uchokozi  maisha na mziki usukuni weka pembeni dereva...

Mama Mwenye Taadhima ; Shairi

Image
Mama Yangu Mama malkia,thamani yake sijaona Mafunzo alonigea, busara na hekima. nani wakufikia, heshima yake mama, Salamu hizi pokea, mama mwenye taadhima. maovu yangu mkuki, hukita moyoni mwako. Hupigwa taharuki, kusema na mola wako. yasinifike mauti, iponywe damu yako. mama wewe  asali, utamu undani yako. Mama, neno tamu, upendo wake hudumu najawa na Tabasamu, jinale halishi hamu, kiumbe maalumu, kaumbwa kitaalamu ninani asofahamu huyu mama ni adhimu itachora jina mama, ikimwagika hii damu! namimi nitalisoma, kwa utashi na nidhamu, kughilibu nitagoma, laana yake ni sumu Nikikosa nitasema, Nisamehe sana mama. Ungali bado wazoni, ingawa u kaburini ila bado naamini upo mwangu maungoni mwenginewe simuoni, wafaraja maishani Penye kosa nakuomba nisamehe sana mama. kipindi tungali sote, hukunifunza  ujinga Ilipangwa uondoke, ningewezaje kupinga si kwamba niadhirike, Mungu bingwa wakupanga ujumbe wangu ufike, mwanao anakupenda. mwisho wa huu utenzi ...

THAMANI YA WAZAZI

Image
Naitwa Omar Bin Zongo, wakati mwengine hua napenda kujiita Bin Zongo sababu yakufananisha thamani ya kilichopo ndani yangu na mimi maana mara zote umbile langu halifanani na busara zangu labda pengine nikimtanguliza baba yangu mbele watu watasema amerithi kwa huyo Zongo. najivunia zaidi na napenda ukiniita Bin Zongo... leo nina ujumbe maridhawa nataka kukugea. Baba yangu alifariki dunia mwaka 1995 mimi nikiwa mdogo sana siijui hata sauti ya mzazi wangu huyo wakiume. mama yangu amefariki mwaka 2014 nikiwa na ufahamu wangu hakika maumivu ya kifo chake bado yangali moyoni mwangu. kuanzia mwaka huo wa 2014 niliishi bila ile nguvu ya faraja itokanayo na kujua kuwa mama au baba yupo nyuma ya hatua zako. hakuna faraja inayofariji kwa kiwango kikubwa sana duniani kama faraja ile yakukutana na magumu ukahisi mama au baba yako atasimama kwako kwa ushauri na hata muongozo mwengine wowote utakaokuwa unauhitaji kutoka kwao. hiyo ndio nguvu itokanayo na tumaini la kujua kuwa wazazi w...

NIMEGHAFIRIKA

Image
Allah mkarimu sana, ana nifanya nahema Nakushukuru kwa sana, kunijazia neema Wewe uliye bayana, hutujuza baya   jema Dunia tambala gani, na nimeghafirika Sikio lazidi kichwa, wahenga hawapo tena Vibiongo   vimefichwa, uwazi haupo tena Vinaliwa tu na mchwa, kwasababu ya   hiyana Dunia tambala gani, na nimeghafirika Wanaitana   vyumbani, mda wa kula fikapo Kwa minong’ono ya chini, wanafungua makopo Na tena pasipo soni, wanazizuia   pepo Dunia tambala gani, na nimeghafirika Dunia sio tambala, halifai hata dekio Ukizubaa kulala, utabaki na masikio Pima umri kabla, ni mingapi masalio Dunia tambala gani, na nimeghafirika Msikia la mkuu, nini amefaidika Amevunjika guu, au hakukumbuka Kuhesabu toka juu, kukwepa kughadhabika Dunia tambala gani, na nimeghafirika Hiyari ni ndoto njema, ukiiota mchana Uking’amua mapema, achana na kubishana Ya nini ukilema, kwa yasiyo na maana Dunia tambala gani, na nimeghafirika...

UMEPATA KILICHO BORA 2016?

Image
 Na Omar Zongo +255 782181862 (watsap) Kwa wale marafiki zangu wapya wa mitandao ya kijamii, wasikilizaji wangu wapya wa redio mlimani na wasomaji wangu wapya wa SIMULIZI ZINAISHI naamini ni ninyi pekee ndio mnaweza mkawa hamuijui hulka yangu ya kuongozwa na msemo katika kila mwaka! wale wandani wangu wakitambo sina shaka hata ukitaka wakumbushie mwaka huu mkongwe wa 2016 tumeongozwa na msemo gani watakwambia tena kwa furaha "tunastahili kilicho bora 2016". mwaka unaisha bado hulka yangu ingali hai mwaka ujao tutaongozwa na kauli nyengine chanya itakayotufanya tuwe na amani kwa mwaka mzima. kabla sijaenda kukupasha kwa vipi mwaka huu tulistahili kilicho bora acha nikumbushie misemo ya miaka yanyuma kidogo ili twende sawa kwako wewe damu yangu ngeni. nitaanzia mwaka 2015 ilikuwa ni CHAGUA KUWA MWEMA na hakika tulikuwa wema haswa nachelea kusema mpaka sasa chembechembe za wema zingali damuni mwangu, hakika nakwambia sijawahi kujutia kuchagua njia ile...

UTOTO ; SHAIRI

Image
Na. Bin Zongo utoto upofu, huyaoni ya dunia, hupenda  unyoofu, yakipinda huchukia, utoto mapungufu,  wazazi huvumilia. utoto kumbe ni hivi, mama yangu nisamehe. nisamehe mama yangu, hakika nilikuudhi. enzi za utoto wangu, sikuitaka ajizi nilipotaka jambo langu ulipaswa kulikidhi, sikuyajali machungu  poleni sana wazazi. poleni sana walezi,  nyie adha mwazijua nimekua siku hizi  namie nayatambua, mgumu sana ulezi,  watoto wanasumbua hasa wasiku hizi, utajuta kuwajua. Utajuta kuwajua  watakacho ndicho hicho werevu wasotambua kama huna ama unacho wataanza kulilia  ukileta kiinimacho wamezaliwa wanajua hawataki danganya toto. mabingwa wakuchagua kipikwe chakula gani, nawewe utaangalia, wakitazama katuni, mada zao kuchangia  itakupasa ukiwa nyumbani. wao ndio hudatia nyumba yote nje ndani. niwao ndio mabosi wewe kijakazi wao, kukusaidia kazi  ni mpaka hiyari yao haweshi ulalamishi wakitaka ...

MASIKINI SINA CHANGU ; SHAIRI

Image
Na Bin Zongo. msimu ndio huu msimu wa siku kuu msimu wenye makuu masikini sina changu. msimu wa usaliti msimu watashtiti msimu wa yakuti masikini sina changu msimu flani wa adha fahari na nyingi bugdha msimu wakuumiza masikini sina changu msimu wakupendeza msimu wakuchombeza msimu wakuumiza masikini sina changu msimu huu wataka kula kunywa nakusaza na pesa zakusakata masikini sina changu msimu wanisaliti wahuba hanitaki ataka mlimani city masikini sina changu mavazi ya kifahari ataka kupanda meli visiwani kuvinjari masikini sina changu msimu wataka nyama kama samaki jodari mfukoni pesa sina masikini sina changu mialiko nayo mingi tatizo langu nauli hali yangu siipingi masikini sina changu gharika limenipiga katika mifuko yangu ukata umenizonga masikini sina changu msimu huu adimu wafaa kupokelewa ila pesa ni muhimu masikini sina changu wazuri wote mashem mie nitawapa nini sina pakwenda sehem masikini sina changu mivinyo yaki...

ANGUKO; SHAIRI

Image
Nina ipata faraja, kwa pendo la maulana Sina gumizi kutaja, kwa nguvu za Subuhana Na giza likisha kuja, kimbilio kwa Rabana Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana Kumbukumbu sifa njema, sipokupa maumivu Ukikumbuka kilema, na ukalishika kovu Mwili utakuzizima, na kupata ukamavu Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana Vunjiko kuu la moyo, halinipi majutio Mengi yavunjikayo, nayaziba masikio Ninayafuata hayo, kupata mafanikio Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana Mimi   wa kuvaa moja,siwezi lilia mbili Ninavikwepa vioja, wanione   wa akili Naliuita umoja, wakaja tukajadili Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana Tukasemezana kucha, lakini hawaku afiki Walifunga na mabucha, utii wa kinafiki Walibaki kula kucha, ni njia za kizandiki Mbishi hana ujanja, kauli yao ya jana Wakabomoa daraja, lilo jengwa vitabuni Na bado wana bwabwaja, hawajui nina   nini Wananiona buwaja, mzamaji wa ziwani Mbishi hana ujanja, kauli y...

CHOZI LAKO ; SHAIRI

Image
Naitafakari siku, ilivyoishia vema Tena Kwa nyingi shauku, nilitamani kusema Na hali yangu kapuku, akili ikazizima Asante kwa chozi lako, nimeijua   thamani A nililiaye nani, kwa uchungu wa mapendo Nalijihisi katuni, tena nisiye vishindo Nitesekae jangwani, nisipate maji fundo Asante kwa chozi lako, nimeijua   thamani Kutangatanga msafiri, nisietua mizigo Ninazipanga safari, zilizo nyingi mitego Sasa natafakari, ingawa mekupa zogo Asante kwa chozi lako, nimeijua   thamani Neno gani nikwambie, huenda ukaelewa Unisikilize mie, tayari nimechachawa Ububu nijivikie, usije ona melewa Asante kwa chozi lako, nimeijua   thamani Nalikutoa machozi, na wala sikukufuta Yalidondoka kwe ngozi, hukutaka kupukuta Nilijifanya ajizi, nisiyejua chakufata Asante kwa chozi lako, nimeijua   thamani Asante kwa chozi lako, limeniweka furahani Najua thamani yako, sitokutoa moyoni Sikuliliwa mwenzako, wewe wa kwanza amini Asante ...

JITU ADUI SEHEMU YA 2

Image
 Na Omar Zongo Walinzi wote walibaki wakimtumbulia macho mtaalamu wa kutambua nyayo, Alionekana kujutia mno kulewa jana yake bila shaka alielewa madhara ya adui aliyepita kuingia duniani. "Huyu adui aliyeingia atagharimu maisha ya vizazi vyetu vijavyo. Watakuwa watukutu, wavivu na watahadaika na mabadiliko ya kasi ya teknolojia kwa kujidanganya ni maendeleo makubwa, lakini kama atapatikana mwerevu na kuhesabu faida ya maendeleo hayo na kurudi kwenye hasara bila shaka atagundua faida ndogo sana dhidi ya hasara. Makosa yetu ya kujisahau usiku wa jana yatagharimu dunia hii!" Alizungumza kwa hisia kali yule mtaalamu wa kutambua nyayo alisema ilikuwa ni habari iliyoibua majuto makuu kwa walinzi wale lakini wangefanyaje sasa na adui keshapenya. Hawakuwa na jinsi tena na ndipo hapo na wao pia walipoanza kupoteza umakini katika kazi yao. Waliendeleza tabia zao za kunywa mvinyo wakijiongopea kuwa wanapoteza mawazo. Maadili ya kazi yao yalishaporwa usiku ule...