Posts

WARAKA WA JPM

Image
 Huu ni waraka wa kufikirika wa Hayati John Pombe Magufuli, Rais awamu ya tano wa Tanzania ambaye alifariki dunia usiku wa tarehe 17 march mwaka 2021... Muandishi wa waraka huu ni Omar Zongo Kutokea Eneo ambalo wanaenda waliokufa tumepokea waraka huu. Waraka wa JPM. Anasema.... Ndugu zangu watanzania,    ile siku ambayo roho yangu iliusaliti mwili wangu, ilikuwa ndio siku ya kwanza ya mimi na ninyi kutenganishwa katika ulimwengu huu wa Roho na Mwili. Sikuwa na namna yoyote ya kupinga rungu la malaika mtoa roho, ninachoshukuru ni kwamba udongo umeudhibiti mwili wangu lakini Roho yangu ingali hai hata kupata uwezo wa kuyaona yanayoendelea Duniani, lakini zaidi kuwaandikia waraka huu. Nimelazimika kuuandika waraka huu kwa sababu nyingi lakini kubwa ni hili tendo linalotarajiwa kujiri hivi karibuni  Tendo la kuuaga mwaka uliogharimu maisha yangu. Najua nimesaliti kiapo cha Uongozi, kwa kuwaacha kabla ya muda, lakini ningewezaje kupinga mapenzi yake Mungu. Katika waraka w...

Kwaheri 2021

 Wakati unakuja tulikupokea kwa Matumaini makubwa na imani yetu ni kwamba nuru ya mafanikio itatuangazia kwa wingi ndani ya siku zako. Matokeo ya tulichoamini na tulichokitumaini ni siri yetu maana ndani yako tumejifunza kuwa kinywa kinachonyamaza kinaiacha na uzima shingo. Walioshindwa kuficha hasadi zao na kutuonyesha wazi chuki walizo nazo juu yetu ni wengi. Kinachoshangaza majina yao ni ya watu ambao mwanzo tuliamini ni majirani wema. Walioacha kutuamini kwa kuhisi ni wazembe na hatujielewi ni wengi pia. Waliongoja tuanguke ili watucheke hawakukosekana na waliotabasamu kinafki kila tuliponana nao tuliwabaini tukakosa cha kuwafanya. Walioacha kupokea simu zetu kwa kuhisi tutawapiga vizinga ni wengi kama idadi ya waliokataa kujibu meseji zetu kwa kujua kuwa tuna shida. Matendo yetu ya wema yaliyopokelewa kama ni shobo na kujionesha ni mengi kama yalivyo malipo ya dhuluma na chuki tulizoambulia. Mifuko yetu iliposhindwa kununua upendo tukaambulia dharau na kupuuzwa. Juhudi zetu za...

ACHA!! USING'ANG'ANIE MAHUSIANO YALIYOISHA MUDA WAKE.

 Kuanzisha mahusiano ya mapenzi sio dhambi wala jambo baya katika akili ya yeyote aliye timamu. Lakini ubaya unakuja jitokeza pale ambapo mnashindwana na kushindwa kuamini kama mmeshindwana hivyo kubaki mnavumiliana, mkikondeshana, kudharauliana, kutukanana, kupigana na wakati mwengine hata kuuana. Jifunze leo hapa kumuacha aende zake, kuitambua,kuiheshimu na kuitumia vizuri siku. Siku ya kuachana. Na. Omar zongo. Hakikisha muda wa kuachana ukifika unafanya hima muachane. Using'ang'anie bidhaa ambayo  imefika tamati Yake ya matumizi. Hiyo tayari ni sumu kukuua si ajabu! Muda wa kuachana una dalili na upo dhahiri. Ukiona tu mambo yamebadilika, upendo umechujuka, taa imezimika, nakusihi ondoka. Hakuna Tena zile 'baby' na 'sweetheart' unaitwa kwa jina lako, au 'Apple' na 'Chocolate' ujue ndio mwisho wako. Kitendo cha 'text' kupungua, zile 'I miss you' kupotea na hakuna kujishtukia ujue muda umewadia. Muda wa kuchokana una nyingi tash...

Kifo chako kikitokea

Image
Kifo chako kikitokea, kitawashtua wanaokujua Na wengi watakulilia lakini zaidi watakaoumia ni wale walio karibu na wewe! Pia kwasasa upo hai,Wapo ambao unawakera nakuwaudhi lakini kwa unafki wao siku hiyo watasema kuwa wewe ni mtu mwema sana. Moja ya fikra zako muda huu upo hai ni labda siku ukifa mzigo wa majukumu yako ataubeba ndugu yako flani, kisa anakuchekea, anawafurahia watoto wako, mke au mume wako. Labda kisa mnasaidiana sana na ushamtendea mema mengi! Unajifariji huenda yeye atavaa viatu vyako, atawasomesha kwa moyo mmoja, atawaongoza nakuwafariji bila Tatizo. Sipingi hisia zako inawezekana zipo sahihi, lakini acha nikufikirishe tofauti kidogo! Tambua kuwa binaadamu tumeumbwa Na unafiki wa asili! Wengi wao waliokufa walijifariji kama wewe lakini matokeo yake watoto wao wanadhalilika, ni ombaomba Na wengine hawana ndoto tena. Au wengine walibahatika kulelewa lakini kwa dhiki Na masimango makubwa, makovu ya mateso waliyopitia wanayakumbuka hadi Leo. Ipo hivyo r...

RUDI KWA MAMA

Image
Na. Omar Zongo Wino huu uliomwagika umeandikwa Na yatima asiye Na baba wala mama! Mwenye machungu ya kumbukumbu kila atazamapo picha za wazazi wake! Mwenye tamaa yakuzungumza Na mama kumwambia anampenda! Nakushauriana na baba jinsi dunia inavyokwenda. Leo wino wangu umebeba dhamira yakukumbusha urudi kwa Mama. Usiseme hakuna sababu yamsingi yakwenda kumsalimia mama! Ukifanyacho kinakupa riziki, mafanikio na utajiri lakini vitu hivyo ni vichungu siku utakapokuwa huwaoni wazazi wako. Siku watakapokuwa mbali Na upeo wa macho yako! Siku nawewe utakapokuwa yatima. Rudi kwamama! Nenda kamwambie unampenda sana! Kaseme nae yote yakwako naumsikilize yote yakwake. Hakikisha anafarijika kwa uwepo wako! Usitoe hata dakika akahisi upweke! Akahisi umemtenga nakuzipa thamani kazi zako au watu wako wengine ulionao. Kumbuka wao wanakuona wamuhimu, mwenye nguvu Na wathamani! Kwasababu ya juhudi za wazazi wako. Walikesha nawewe ulipokuwa unawasumbua ukilia usiku kucha enzi ...

'Watu'

Image
Kwa tabu sana Mzee alijisogeza juu ya kitanda nakulaza shingo yake kwenye mto. Uchovu wa maradhi ulimdhoofisha vyakutosha, macho yake yaliashiria kukata tamaa, lakini alijikaza kiume. Alinitazama Na kisha akasema. "Ilikuwa ni siku ambayo kila mtu alinisema vibaya nakunizungumzia vibaya, lawama za kila rangi nilipakwa, Hakuna aliyejuwa niwapi nimeelekea nawewe, ulikuwa bado mchanga kabisa. Nimimi pekee ndio nilijua dhamira yakutoroka nawewe siku ile, Kwakweli Siku ile nilikuwa naingojea kwa hamu sana ifike sababu nilidhamiria kuzungumza nawewe. Nilitoroka nawewe nikaenda mbali kidogo Na nyumba yetu, Ulikuwa una siku 40 tu tangu uzaliwe, nafikiri ndio maana watu walinishangaa sana kuondoka nawewe, tena bila kuwaaga. Nilienda nawewe mahala nilipopajua mwenyewe, Ninachoshukuru nikwamba nilichodhamiria kilifanikiwa. Nilizungumza yote na naamini uliyasikia maana hata kawaida yako yakulia siku ile sikuiona kabisa. Ulinyamaza tuli kana kwamba ulikuwa mkubwa kumbe n...

Tafakari Wengine

Image
Muda mwingi hua unautumia kutafakari mazuri yako huku ukihitaji kusifiwa, hua unatamani kuongelewa wewe tu, unatamani kuonekana  Na wote wanaokuzunguka wasifu nakukuheshimu.  Ni nadra sana mtu kutoa nafasi yakutafakari wengine, hivi ndivyo tulivyoumbwa, tumeumbwa na umimi. Unajiona Bora kuliko wengine, wewe ndio unajiona mwenye akili, busara Na ushauri mzuri unaweza kutokea kwako. Ni ajabu sana tabia hii Na kwa vile ni asili ya kuumbwa kwako sina lawama katika hilo Ila leo nataka utenge muda kutafakari wengine, kuona vipawa vyao, nafasi yao, akili zao Na tamaa zao. Ndio, Anza sasa kumfikiria mtu wako wakaribu, ana umuhimu gani kwako. Acha kuwaza wewe tu ndio mwenye umuhimu kwake. Jiulize maswali ya Je ni vipi ingekuwa kama yeye asingekuwepo. Tuanze Na msaidizi wako wa kazi za ndani. Yeye anafua nguo zako, anakupikia, anakufanyia usafi wa nyumba n.k. Acha kiburi chakusema hata kama asingekuwepo ungetafuta mwengine fikiria kuna watu duniani wanatafuta msa...